Habari njema kwa mashabiki wa Simba ni kuwa wanakaribia kuwashuhudia mabeki wao Wilson Nangu na Abdulrazak Hamza ambao wamekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Mabeki hao wa kati wamekosekana tangu msimu uliopita kutokana na majeraha waliyopata mwanzoni mwa msimu na kupelekea wakafanyiwe upasuaji nje ya nchi.
Lakini baada ya muda mrefu wa kufanya mazoezi binafsi, hatimaye wachezaji hao wameanza kushiriki mazoezi ya timu.
Nangu na Hamza ni sehemu ya wachezaji wa Simba wanaoendelea na mazoezi Polokwane Afrika Kusini katika kambi ya siku 10.

Pengine ni suala la muda wachezaji hao wataanza kuonekana tena na Wanamsimbazi.
Hata ni wazi watahitaji muda kupata utimamu wa mwili kutokana na muda mrefu waliokaa nje ya uwanja.
Aidha watakuwa na kazi ya ziada kuzirejesha nafasi zao kwenye kikosi cha kwanza kwa sasa Ismail Toure na Rushine de Reuck wamejimilikisha nafasi hizo