Mchezo wa Mbeya City v Simba waingiza Mil 74

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Nov 2017
Mchezo wa Mbeya City v Simba waingiza Mil 74
Mechi ya Mbeya City dhidi ya Simba iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya mwishoni mwa wiki imeiingiza Sh74.6 milioni.

Mapato hayo yameshindwa kuvunja rekodi iliyowekwa kwenye uwanja huo wakati Mbeya City ilipocheza na Simba kwa mara kwanza Sh 105 milioni katika msimu wa 2012-13.

Katibu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Mbeya, (Mrefa), Haroub Selemani alisema katika mgawao wa mapato hayo, City imejipata kitita cha Sh23.663 milioni na Simba walipata Sh11.831 milioni.

Selemani alisema kiasi kilichobaki kilikwenda kwa wamiliki wa uwanja Sh8.873 milioni, kodi Sh11.381 milioni, Shirikikisho la Soka Tanzania (TFF) sh2.957 milioni, Bodi ya ligi (TPLB) Sh5.324 milioni, Baraza la Michezo Tanzania (BMT) sh591,578 Chama cha Soka Mkoa (Mrefa) Sh1.774 milioni na gharama za mchezo Sh4.141 milioni.

Ò€œHii kwa kweli imevunja rekodi ukiachana na mechi ya kwanza kabisa ya Mbeya City ilipochezwa hapa baada ya kupanda daraja. Lakini miaka mingine yote hatujawahi zidisha Sh40 milioni,Ò€ alisema Selemani.

"Hata hivyo uwanja wetu haupo katika mazingira mazuri sana tungeweza kupata zaidi ya kiasi hicho. Kwa mfano hili eneo la jukwaa kuu tungeweka uzio ambao linakuwa na kiingilio chake na upande mwingine unakua na kiingilio chake na mageti ya kuingilia yanakuwa tofauti," alisisitiza kiongozi huyo wa MRFA.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’