Msimu mpya wa ligi kuu ya Wanawake uko mbioni kuanza ambapo mapema leo TFF iliweka hadharani ratiba ya mechi za Ngao ya Jamii zitakazopigwa mwishoni mwa mwezi huu.
Kulingana na ratiba hiyo, mabingwa wa ligi ya Wanawake msimu uliopita Simba Queens watacheza dhidi ya watani zao Yanga Princess kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo.
Mechi zote ztapigwa Septemba 30 ambapo mchezo wa mapema wa nusu fainali ya kwanza ni kati ya JKT Queens dhidi ya Mashujaa Fc utakaopigwa saa 9 Alasiri na kufuatiwa na Kariakoo Derby hiyo ya kinadada itakayopigwa saa 12 jioni.
Baada ya kukosa tiketi ya kucheza ligi ya mabingwa, Simba Queens sasa inarejea nyumbani kwa nguvu ikiwa na dhamira ya kukaribisha msimu mpya kibabe.

ADVERTISE HERE