Gueye aandaliwa mkataba mpya mapema Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Sep 2026
Gueye aandaliwa mkataba mpya mapema Simba

Uongozi wa Simba umeanza kuchukua hatua za mapema kuhakikisha unamfunga Libasse Gueye kwa mkataba wa muda mrefu zaidi, huku kiungo huyo mshambuliaji akiendelea kuonyesha umuhimu wake ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.

Gueye amekuwa miongoni mwa wachezaji wanaoonekana zaidi katika mwanzo wa msimu wa 2026/27, akihusika moja kwa moja katika kutengeneza mabao ya Simba.

Katika michezo ya mwanzo ya Ligi Kuu, nyota huyo wa Senegal amefunga bao moja na kutoa pasi tano za mwisho, huku pia akipachika mabao mawili kwnye ligi ya mabingwa takwimu zinazomweka kuwa mchezaji mwenye mchango mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya Simba.

Simba haitaki kusubiri

Taarifa za ndani zimebainisha kuwa Simba haipo tayari kusubiri hadi mkataba wake ufikie hatua za mwisho kabla ya kuanza mazungumzo.

Gueye bado ana mkataba wa mwaka mmoja na zaidi Simba, lakini kiwango alichoanza nacho msimu huu pamoja na kuvutia kwa kwake katika dirisha lililopita, kumeifanya klabu hiyo kutaka kuweka mambo sawa mapema.

Inaelezwa Simba imeanza mazungumzo ya kuongeza mkataba wa Gueye, huku ikitajwa kuwa klabu hiyo iko tayari kumpa maboresho ya kifedha ili kumshawishi kuendelea kubaki Msimbazi.

Hatua hiyo inaeleweka zaidi ukizingatia kwamba Gueye amekuwa akitajwa na klabu mbalimbali za Afrika na Ulaya katika kipindi cha usajili.

Walimfuata, Simba ikaweka ngumu

Kabla ya msimu huu kuanza, kulikuwa na taarifa za klabu kadhaa kuonyesha nia ya kumsajili Gueye.

Miongoni mwa klabu zilizokuwa zimeonyesha kuvutiwa naye ni MC Alger, Esperance na klabu kadhaa kutoka barani Ulaya (Uturuki). 

Ukiangalia mwanzo wa msimu, Gueye amekuwa akithibitisha kwa vitendo kwa nini Simba iliamua kumzuia.

Ana uwezo wa kucheza katika maeneo tofauti ya safu ya ushambuliaji, huku ubunifu wake ukiwa moja ya silaha zinazosaidia Simba kuvunja ulinzi wa wapinzani.

Asisti tano katika mechi za mwanzo za ligi zinaonyesha zaidi ya uwezo wa kufunga; zinaonyesha pia namna anavyohusika katika kuandaa mabao kwa wenzake.

Ndiyo maana uongozi wa Simba unaonekana kutaka kumuweka salama mapema kabla thamani yake ya sokoni haijaendelea kupanda.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’