Msimu hana haraka Simba, anaendelea kujifunza

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Sep 2026
Msimu hana haraka Simba, anaendelea kujifunza

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Bakari Selemani Msimu, amesema hatua ya kujiunga na klabu hiyo imemfungulia nafasi ya kujifunza kwa kiwango kikubwa kutokana na ushindani uliopo ndani ya kikosi cha Wanamsimbazi.

Msimu alijiunga na Simba katika msimu huu akitokea Coastal Union, klabu iliyomlea tangu akiwa kwenye timu za vijana kabla ya kumpandisha katika kikosi cha wakubwa. Akiwa Coastal Union, alifanikiwa kufunga mabao manne katika msimu wa 2024/25 na matatu msimu uliofuata.

Licha ya kutokuwa mchezaji wa kudumu katika kikosi cha kwanza cha Simba kwa sasa, Msimu anaona hali hiyo kama sehemu ya mchakato wa kujenga uwezo wake badala ya kuwa sababu ya kukata tamaa.

Mchezaji huyo amesema mazingira anayokutana nayo Simba yamemsaidia kuongeza uelewa wake katika maeneo mbalimbali ya mchezo, hususan upande wa ufundi, mbinu pamoja na namna ya kujiandaa kupitia mazoezi.

Ametaja uwepo wa wachezaji wenye uzoefu na viwango vya juu ndani ya Simba unampa fursa ya kujifunza moja kwa moja kutoka kwa mastaa hao huku akiendelea kupigania nafasi yake.

Msimu, ambaye huu ni msimu wake wa tatu kwenye Ligi Kuu tangu alipopandishwa katika kikosi cha wakubwa, tayari amepata nafasi ya kuonekana katika michezo mitatu ya Simba msimu huu.

Alitumika kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, na pia akipewa nafasi katika michezo ya ligi dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’