Wakati kikosi cha Simba kikitarajiwa kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kambi ya siku 10, takribani wachezaji saba watakuwa kwenye majukumu ya kimataifa.
Wachezaji hao wamejumuishwa kwenye timu za Taifa kwa ajili ya mechi za kuwania tiketi ya Afcon 2027.
Nyota hao ni pamoja na Yusuf Kagoma, Vedastus Masinde, Bakari Msimu, Anthony Mligo, Nathaniel Chilambo, Morice Abraham na Djibrilla Kassali aliyejiunga na timu ya Taifa ya Niger.
Hata hivyo unaweza kusema hakuna litakaloharibika kwani wachezaji hao wataendelea na program za mazoezi wakiwa timu za Taifa na watarejea wakiwa kwenye ari ya ushindani.
Habari njema kwa Simba pia ni kuwa mastaa wake muhimu wengi hawatakuwa na majukumu ya timu za Taifa hivyo kocha Steve Barker atakuwa na wasaa mzuri wa kukiandaa kikosi chake akiwa na silaha zake kamili.
Nyota kama Clatous Chama, Anicet Oura, Libasse Gueye, Rushine de Reuck, Ismail Toure, Ibrahim Jaabar, Keletso na wengine wanatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoelekea Afrika Kusini kuweka kambi ya siku 10 kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga na ratiba ya mechi nyingine za ligi kuu na ligi ya mabingwa.