Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kimefanikiwa kuondoka na alama moja dimba la Mandela huko Uganda baada ya kulazimisha suluhu ya bila kufungana na wenyeji wao Uganda Cranes.
Licha ya mazingira mabaya ya uwanja kutokana na mvua kubwa iliyonyesha muda mfupi kabla ya mchezo, vijana wa Stars waliweza kumudu mikiki mikiki ya wenyeji wao waliokuwa wakishangiliwa na maelfu ya mashabiki wao waliofurika dimba la Mandela.
Kipindi cha kwanza hakikuwa kizuri sana kwa Stars kwani Uganda ilipeleka mashambulizi mengi langoni mwa Tanzania hivyo kufanya safu ya ulinzi kufanya kazi ya ziada kuzuia mashambulizi hayo yaliyoongozwa na Emanuel Okwi na Farouq Miya..
Hata hivyo kwenye kipindi cha pili Stars ilizinduka na kutengeneza nafasi kadhaa za mabao kupitia kwa washambuliaji wake Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Saimon Msuva.
Samatta alikosa moja ya nafasi za wazi za mchezo huo huku pia akipiga mpira wa adhabu uliopita sentimeta chache langoni mwa Uganda.
Matokeo hayo ya sare ni mazuri kwa Stars iliyokuwa ugenini na sasa imefikisha alama mbili.
Uganda inaendelea kubaki kileleni mwa kundi L baada ya kufikisha alama nne.
Lesotho na Cape Verde timu nyingine za kundi L zitachuana kesho kwenye mchezo mwingine wa michuano hiyo ya kusaka tiketi ya fainali za AFCON 2019.
Stars imebakisha michezo miwili ya ugenini dhidi ya Lesotho na Cape Verde na michezo miwili ya nyumbani dhidi ya Uganda na Cape Verde.

ADVERTISE HERE