Barker aendeleza rekodi ya kutisha Ligi Kuu, mechi 31 bila kupoteza

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Sep 2026
Barker aendeleza rekodi ya kutisha Ligi Kuu, mechi 31 bila kupoteza

Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ameendelea kuweka rekodi yake nzuri katika Ligi Kuu ya NBC baada ya juzi kuiongoza timu hiyo kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Ushindi huo umeifanya Barker kufikisha mechi 31 mfululizo za Ligi Kuu bila kupoteza tangu alipojiunga na Simba, huku akishuhudia timu yake ikishinda michezo 24 na kutoka sare mara saba katika kipindi hicho.

Katika michezo hiyo, Simba imekusanya pointi 79, imefunga mabao 54 na kuruhusu mabao 10 pekee, jambo linaloonyesha mwendelezo wa matokeo mazuri chini ya kocha huyo raia wa Afrika Kusini.

Mchezo dhidi ya Azam ulikuwa muhimu katika kuendeleza rekodi hiyo, huku Simba ikilazimika kusubiri hadi kipindi cha pili kupata mabao yake mawili.

Azam ilijifunga katika dakika ya 58 baada ya mpira wa kona uliopigwa na Nathaniel Chilambo kuleta taharuki ndani ya eneo la hatari, kabla ya Clatous Chama kuongeza bao la pili dakika ya 67.

Matokeo hayo yameendelea kuipa Simba mwendelezo mzuri katika kampeni zake za Ligi Kuu msimu huu ikishinda mechi zote sita, huku Barker akiongeza idadi ya michezo ambayo hajapoteza tangu alipokabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo.

Barker alijiunga na Simba Desemba 2025 akitokea Stellenbosch ya Afrika Kusini, klabu ambayo alikuwa ameijenga kuwa moja ya timu zinazoshindana kwa nguvu katika soka la nchi hiyo.

Tangu alipowasili Msimbazi, kocha huyo ameendelea kupata matokeo chanya katika ligi, huku safu yake ya ulinzi ikionyesha uimara kwa kuruhusu mabao 10 pekee katika mechi hizo 31.

Kwa upande wa mashambulizi, Simba imefunga mabao 54 katika kipindi hicho, wastani wa zaidi ya bao moja na nusu kwa kila mchezo.

Ushindi dhidi ya Azam pia umeendeleza mwanzo mzuri wa Simba katika msimu huu, huku timu hiyo ikiendelea kujiweka vizuri katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’