Kikosi cha Simba kintarajiwa kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya ligi kuu dhidi ya Yanga pamoja na mechi nyingine zitakazofuata baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA.
Ligi imesimama kwa takribani wiki tatu ambapo ni kipindi kirefu kinachohitaji mkakati wa maandalizi ili kuhakikisha timu inaendelea kusalia kwenye ushindani.
Taarifa za ndani zimebainisha kuwa Rais wa heshima wa Simba Bilionea Mohamed Dewji 'Mo' ameidhinisha mpango huo akigharamia mahitaji yote ya kambi hiyo.
Msimu huu Simba imeweka malengo makubwa ambapo mkakati ni kulisaka taji la ligi kuu ambalo wamelipoteza kwa misimu mitano sasa.
Lakini pia Mnyama amelenga kufanya vyema zaidi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa baada ya kampeni isiyoridhisha msimu uliopita.