Barker kuweka mkakati wa ushindi Dabi ya Kariakoo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Sep 2026
Barker kuweka mkakati wa ushindi Dabi ya Kariakoo

Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam Fc, nyota wa Simba watakuwa na mapumziko ya siku chache kabla ya kuanza maandalizi kuelekea mchezo unaofuata dhidi ya Yanga.

Kwa sasa ligi imesimama kwa takribani wiki tatu kupisha kalenda ya FIFA ambapo pale itakaporejea, itakaribishwa na mchezo wa Dabi ya Kariakoo.

Mkufunzi wa Simba Steve Barker ameweka wazi dhamira yake ni kuona wanashinda mchezo huo akitarajiwa kutumia kipindi hiki cha mapumziko kukiandaa vyema kikosi chake.

Barker ana imani Simba itakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kushinda mchezo huo kwa sababu wachezaji wake wamezoeana wakiwa pamoja tangu msimu uliopita na wamedhihirisha kwa kufanya vyema katika mechi zilizopita ambapo kikosi kimeshinda mechi nane mfululizo kwenye mashindano yote.

"Asilimia kubwa ya wachezaji waliopo Simba walikuwepo tangu msimu uliopita, wana uzoefu mkubwa na mechi ya aina hiyo, lakini kikosi kimekuwa na mwendelezo wa kufanya vizuri, hilo linanipa nguvu ya kuamini mchezo utakuwa mzuri na tunaweza kupata pointi tatu”

 “Nafahamu hautakuwa mchezo mwepesi lakini kwa sasa wachezaji wanastahili mapumziko haya machache ya FIFA ili kupumzika, kujipanga upya na kuongeza nguvu, kisha tutarudi tena uwanjani kuendeleza mapambano ya ligi,” alisema Barker

Katika kipindi hiki Simba itawakosa baadhi ya wachezaji ambao wanakwenda kwenye majukumu ya timu za Taifa.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’