Kuelekea mchezo wa mkondo wa pili hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) kati ya Simba dhidi ya Mighty Wonderers, viingilio vya mchezo huo vimetangazwa.
Jumapili Septemba 13 dimba la Uhuru litawashuhudia mashabiki wa Simba wakiujaza uwanja huo katika mchezo ambao Wekundu wa Msimbazi watakuwa wakisaka matokeo ya ushindi ili kutinga raundi ya kwanza.
Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0 waliopata ugenini, Malawi.
