Klabu ya Simba imethibitisha kuwa kiungo wake, Libasse Geye, amemaliza adhabu yake ya kadi nyekundu katika mashindano ya CAF na anaruhusiwa kurejea kwenye kikosi kitakachokutana na Mighty Wanderers katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Akizungumza, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema Libasse alimaliza adhabu yake baada ya kukosa mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika, huku beki Shomari Kapombe akiwa bado anapaswa kutumikia adhabu yake.
Libasse alionyeshwa kadi nyekundu baada ya mchezo dhidi ya Petro de Luanda uliochezwa Februari 7, 2026 nchini Angola na kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Ahmed amesema tukio hilo lilitokea baada ya mchezo kumalizika, tofauti na Kapombe ambaye alitolewa wakati mchezo ukiendelea.
Kwa mujibu wa Ahmed, tukio lililosababisha kadi hiyo lilihusisha pia mchezaji wa Simba, Alassane Kante, lakini waamuzi walimchukulia hatua Libasse.
Kutokana na adhabu hiyo, Libasse alikosa michezo miwili ya Ligi ya Mabingwa Afrika; dhidi ya Stade Malien katika msimu wa 2025/26 na dhidi ya Mighty Wanderers katika hatua ya kwanza ya msimu wa 2026/27.
Hivyo, kurejea kwa Libasse kunampa Simba chaguo jingine muhimu katika eneo la kiungo wakati timu hiyo ikijiandaa kwa mchezo wa marudiano dhidi ya Mighty Wanderers.
Kwa upande mwingine, Kapombe ambaye pia ni majeruhi, bado hajaimaliza adhabu yake ya kukosa mechi tatu, hivyo atawakosa Mighyty Wonderers