Baada ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha Simba leo kinarejea mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa mkondo wa pili hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Mighty Wonderers.
Jumapili Septemba 13 Simba itakuwa mwenyeji wa Mighty Wonderers katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Kikosi cha kocha Steve Barker kimedhamiria kumaliza kazi iliyobaki dimba la Uhuru baada ya ushindi wa bao 1-0 ugenini.
Simba inahitaji ushindi au matokeo yoyote ya sare ili kufuzu raundi ya kwanza.