Mpya

Bado hatujamaliza kazi - Magori

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3d ago
Bado hatujamaliza kazi - Magori

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Crescentius Magori amesema ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mighty Wonderers katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika ni hatua nzuri lakini badi wanapaswa kumaliza kazi kwenye mchezo wa marudiano.

Akizungumza muda mfupi baada ya kikosi cha Simba kurejea jijini Dar es salaam wakitokea Malawi, Magori aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Uhuru siku ya Jumapili ili kuhakikisha wanamaliza kazi iliyobaki pamoja.

"Mchezo ulikuwa mgumu, Mighty Wonderers ni timu nzuri tunafurahi tumewezakupata ushindi ugenini lakini kazi bado hatujaimaliza"

"Tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi uwanja wa Uhuru siku ya Jumapili ili tukamilishe mpango wetu wa kufuzu hatua inayofuata," alisema Magori.

Simba itakuwa na siku 6 za kukamilisha maandalizi yake kuelekea mchezo huo wa mkondo wa pili utakaopigwa Septemba 13 uwanja wa Uhuru, saa 10 jioni.

More Stories

Simba yakamilisha maandalizi dimba la Uhuru
Simba yakamilisha maandalizi dimba la Uhuru
4h ago
READ MORE β†’
Libasse ameweka kabatini tuzo ya kwanza ya ligi kuu msimu huu
Libasse ameweka kabatini tuzo ya kwanza ya ligi kuu msimu huu
7h ago
READ MORE β†’
Mighty Wonderes wawasili Dar usiku
Mighty Wonderes wawasili Dar usiku
11h ago
READ MORE β†’
Makgalwa ajipa muda zaidi Simba
Makgalwa ajipa muda zaidi Simba
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
14h ago
READ MORE β†’
Mighty Wonderers kutua nchini leo, Simba yawaandalia dozi
Mighty Wonderers kutua nchini leo, Simba yawaandalia dozi
1d ago
READ MORE β†’
Kibabage ameanza mazoezi mepesi
Kibabage ameanza mazoezi mepesi
1d ago
READ MORE β†’
Chama apotezea kelele za mitandaoni, aweka msimamo
Chama apotezea kelele za mitandaoni, aweka msimamo
1d ago
READ MORE β†’
Oura anaamini huu utakuwa msimu bora kwa Simba
Oura anaamini huu utakuwa msimu bora kwa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Septemba 10 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Septemba 10 2026
1d ago
READ MORE β†’