Kikosi cha Simba SC kimerejea nchini usiku wa Jumatatu, Septemba 7, 2026, kikitokea Malawi ambako juzi walijihakikishia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mighty Wanderers katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali.
Mnyama amerejea nyumbani akiwa na faida ya bao moja kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumapili, Septemba 13, 2026, katika Uwanja wa Uhuru.
Ushindi huo wa ugenini umeiweka Simba katika nafasi nzuri ya kusonga mbele, lakini kocha mkuu wa Simba Steve Barker amesema kazi bado haijaisha. Kikosi hicho sasa kinarejea kwenye maandalizi ya mchezo wa pili kwa lengo la kupata matokeo yatakayokihakikishia tiketi ya hatua inayofuata.
Barker awataka mashabiki kuijaza Uhuru
Akizungumza baada ya kurejea nchini, Barker, amesema timu yake inahitaji kucheza kwa umakini na kuhakikisha inapata matokeo yatakayoiwezesha kufikia hatua inayofuata ya mashindano hayo.
Barker pia ametoa wito kwa mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Uhuru Jumapili, akiamini kuwa sapoti kutoka kwa mashabiki inaweza kuwa kichocheo muhimu kwa wachezaji wakati wa kuwania ushindi.
“Tunawaomba mashabiki waje kwa wingi. Uwepo wao utawapa wachezaji hamasa kubwa katika mchezo huu muhimu,” Barker amesisitiza.
Libasse Gueye kurejea kikosini
Katika hatua nyingine, kiungo mshambuliaji Libasse Gueye amemaliza adhabu ya kadi nyekundu na atakuwa tayari kuikabili Mighty Wonderers kwenye mchezo wa marudiano.
Barker amethibitisha kuwa Barker amemaliza adhabu na atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Mighty Wonderers Jumapili.