Kikosi cha Simba kimeondoka Malawi kurejea Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa mkondo wa pili hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Mighty Wonderers utakaopigwa Jumapili Septemba 13 uwanja wa Uhuru.
Simba itakuwa na muda wa kutosha kujiandaa na mchezo huo ambao Wekundu wa Msimbazi watahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili kutinga raundi ya kwanza.





