Klabu ya Simba imethibitisha kuwa mchezo wa mkondo wa pili hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Mighty Wonderers utapigwa uwanja wa Uhuru. Mchezo huo utapigwa Jumapili Septemba 13, saa 10 jioni.
Simba itaingia kwenye mchezo huo ikihitaji ushindi au matokeo yoyote ya sare ili kutinga raundi ya kwanza baada ya ushindi wa bao 1-0 ugenini.
