Mpya

Kassali ana asisti ligi ya mabingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4d ago
Kassali ana asisti ligi ya mabingwa

Mlinda lango wa Simba Djibrilla Kassali jana alikuwa silaha muhimu ya Wekundu wa Msimbazi katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mighty Wonderers katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL).

Kassali jana alidhihirisha kwa nini uamuzi wa uongozi wa Simba kumuongezea mkataba ulikuwa na maana kubwa kwani alihusika katika ushindi huo kwa asilimia 100.

Ni mara chache kusikia mlinda lango anatoa asisti, ndicho alichofanya Kassali jana kwani mpira wake mrefu ulitndewa haki na winga Anicet Oura akiifungia Simba bao muhimu ugenini ambalo liliwahakikishia Wekundu wa Msimbazi ushindi na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu raundi inayofuata kwenye michuano hiyo.

Lakini pia Kassali alifanya kazi kubwa langoni akiokoa michomo kadhaa ya hatari iliyoelekezwa kwake.

Wakati mchezo ukielekea ukiongoni, Mighty Wonderers waliongeza presha kusaka bao la kusawazisha lakini unaweza kusema kikwazo kikubwa kwao alikuwa Kassali akishirikiana vyema na safu ya ulinzi.

More Stories

Simba yakamilisha maandalizi dimba la Uhuru
Simba yakamilisha maandalizi dimba la Uhuru
11h ago
READ MORE β†’
Libasse ameweka kabatini tuzo ya kwanza ya ligi kuu msimu huu
Libasse ameweka kabatini tuzo ya kwanza ya ligi kuu msimu huu
14h ago
READ MORE β†’
Mighty Wonderes wawasili Dar usiku
Mighty Wonderes wawasili Dar usiku
18h ago
READ MORE β†’
Makgalwa ajipa muda zaidi Simba
Makgalwa ajipa muda zaidi Simba
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
21h ago
READ MORE β†’
Mighty Wonderers kutua nchini leo, Simba yawaandalia dozi
Mighty Wonderers kutua nchini leo, Simba yawaandalia dozi
1d ago
READ MORE β†’
Kibabage ameanza mazoezi mepesi
Kibabage ameanza mazoezi mepesi
1d ago
READ MORE β†’
Chama apotezea kelele za mitandaoni, aweka msimamo
Chama apotezea kelele za mitandaoni, aweka msimamo
1d ago
READ MORE β†’
Oura anaamini huu utakuwa msimu bora kwa Simba
Oura anaamini huu utakuwa msimu bora kwa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Septemba 10 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Septemba 10 2026
1d ago
READ MORE β†’