Mpya

Gueye awapa mzuka wachezaji Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5d ago
Gueye awapa mzuka wachezaji Simba

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Libasse Gueye, amewapa mzuka wachezaji wenzake kuelekea mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mighty Wanderers ya Malawi, licha ya yeye kukosekana kwenye mchezo huo utakaopigwa leo Jumapili saa 10:00 jioni.

Gueye amesema mwenendo mzuri wa Simba katika Ligi Kuu Bara, ikiwemo ushindi wa michezo mitano mfululizo, umeongeza nguvu, morali na kujiamini kwa kikosi hicho kuelekea kuanza kwa safari yao ya kimataifa.

Gueye amesema matokeo hayo mazuri yamekuwa sehemu muhimu ya maandalizi ya Simba kabla ya kukutana na Mighty Wanderers, huku akiamini wachezaji wenzake wana uwezo wa kuendeleza kasi hiyo kwenye michuano ya kimataifa.

“Ushindi wa michezo mitano mfululizo umetupa nguvu na kujiamini zaidi. Tunaingia kwenye mchezo huu tukiwa na morali kubwa na tukiwa tayari kupambana,” Gueye amesisitiza.

Gueye hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba leo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata msimu uliopita katika mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Petro Atletico ya Angola.

Kutokuwepo kwake ni pigo kwa upande wa Simba, lakini kauli yake imeongeza hamasa ndani ya kikosi huku akiwataka wachezaji wenzake kutumia nafasi hiyo kuonyesha ubora wao kwenye jukwaa la Kimataifa.

More Stories

Simba yakamilisha maandalizi dimba la Uhuru
Simba yakamilisha maandalizi dimba la Uhuru
7h ago
READ MORE β†’
Libasse ameweka kabatini tuzo ya kwanza ya ligi kuu msimu huu
Libasse ameweka kabatini tuzo ya kwanza ya ligi kuu msimu huu
10h ago
READ MORE β†’
Mighty Wonderes wawasili Dar usiku
Mighty Wonderes wawasili Dar usiku
14h ago
READ MORE β†’
Makgalwa ajipa muda zaidi Simba
Makgalwa ajipa muda zaidi Simba
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mighty Wonderers kutua nchini leo, Simba yawaandalia dozi
Mighty Wonderers kutua nchini leo, Simba yawaandalia dozi
1d ago
READ MORE β†’
Kibabage ameanza mazoezi mepesi
Kibabage ameanza mazoezi mepesi
1d ago
READ MORE β†’
Chama apotezea kelele za mitandaoni, aweka msimamo
Chama apotezea kelele za mitandaoni, aweka msimamo
1d ago
READ MORE β†’
Oura anaamini huu utakuwa msimu bora kwa Simba
Oura anaamini huu utakuwa msimu bora kwa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Septemba 10 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Septemba 10 2026
1d ago
READ MORE β†’