Mpya

Matchday; Mighty Wonderers vs Simba, CAF CL PR1

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5d ago
Matchday; Mighty Wonderers vs Simba, CAF CL PR1

Simba Sc leo inashuka kwenye Uwanja wa Bingu jijini Lilongwe kuvaana na wenyeji wao Mighty Wonderers, katika mchezo wa kwanza wa raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAFCL).

Mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, unatajwa kuwa mtihani mzito kwa wenyeji wanaokabiliwa na rekodi bora ya kimataifa ya Simba SC katika miaka ya hivi karibuni.

Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ameweka wazi kuwa timu yake haikuja Malawi kutafuta sare, bali kupambana kupata ushindi utakaowarahisishia kazi katika mchezo wa marudiano utakaopigwa jijini Dar es Salaam.

Simba imeingia vitani ikiwa na morali kubwa baada ya kushinda mechi zake tano zilizopita za mashindano ya ndani.

Mighty Wanderers wao wanatarajiwa kutumia faida ya uwanja wa nyumbani na mashabiki wao kujaribu kupata matokeo chanya.

Timu hiyo inapitia kipindi cha mpito kwenye benchi lao la ufundi na matokeo yanayosuasua kwenye ligi ya ndani, ni wazi leo watakuwa na kazi kubwa mbele ya Wekundu wa Msimbazi.

Mchezo huu utachezwa chini ya mwamuzi wa kimataifa Charles Bulu kutoka nchini Ghana, na utarushwa mubashara kupitia chaneli ya Azam Sports 2 HD.

More Stories

Simba yakamilisha maandalizi dimba la Uhuru
Simba yakamilisha maandalizi dimba la Uhuru
8h ago
READ MORE β†’
Libasse ameweka kabatini tuzo ya kwanza ya ligi kuu msimu huu
Libasse ameweka kabatini tuzo ya kwanza ya ligi kuu msimu huu
11h ago
READ MORE β†’
Mighty Wonderes wawasili Dar usiku
Mighty Wonderes wawasili Dar usiku
14h ago
READ MORE β†’
Makgalwa ajipa muda zaidi Simba
Makgalwa ajipa muda zaidi Simba
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
18h ago
READ MORE β†’
Mighty Wonderers kutua nchini leo, Simba yawaandalia dozi
Mighty Wonderers kutua nchini leo, Simba yawaandalia dozi
1d ago
READ MORE β†’
Kibabage ameanza mazoezi mepesi
Kibabage ameanza mazoezi mepesi
1d ago
READ MORE β†’
Chama apotezea kelele za mitandaoni, aweka msimamo
Chama apotezea kelele za mitandaoni, aweka msimamo
1d ago
READ MORE β†’
Oura anaamini huu utakuwa msimu bora kwa Simba
Oura anaamini huu utakuwa msimu bora kwa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Septemba 10 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Septemba 10 2026
1d ago
READ MORE β†’