Mpya

Barker aahidi soka safi na ushindi Malawi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Sep 2026
Barker aahidi soka safi na ushindi Malawi

Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker amesema kikosi chake kiko Malawi kikiwa na dhamira moja tu, kuonyesha soka safi na kupata ushindi kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Mighty Wonderers.

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo wa hatua ya awali utakaopigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa Bingu, Barker amesema anatambua wanakutana na timu nzuri ambayo ina wachezaji wenye uzoefu ambao pia wako kwenye timu mbalimbali za Taifa.

Hata hivyo amesisitiza kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo na wanalenga kupata matokeo mazuri ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele raundi inayofuata.

"Kila timu iliyoko kwenye michuano hii inataka kuvuka na kusonga mbele kama ilivyo kwetu Simba."

"Mighty Wonderers ni timu nzuri inayoundwa na wachezaji wengi wenye uzoefu na wako katika timu zao za Taifa."

"Lakini sisi tuko hapa kwa ajili ya kuonyesha soka safi na kupata matokeo chanya," alisema Barker.

Kikosi cha Simba kiliwasili Malawi mapema jana ambapo jioni walipata nafasi ya kufanya mazoezi ya kwanza nchini humo.

Leo Simba itakamilisha maandalizi yake ya mwisho kwenye uwanja wa Bingu.

More Stories

Simba yakamilisha maandalizi dimba la Uhuru
Simba yakamilisha maandalizi dimba la Uhuru
5h ago
READ MORE β†’
Libasse ameweka kabatini tuzo ya kwanza ya ligi kuu msimu huu
Libasse ameweka kabatini tuzo ya kwanza ya ligi kuu msimu huu
8h ago
READ MORE β†’
Mighty Wonderes wawasili Dar usiku
Mighty Wonderes wawasili Dar usiku
12h ago
READ MORE β†’
Makgalwa ajipa muda zaidi Simba
Makgalwa ajipa muda zaidi Simba
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mighty Wonderers kutua nchini leo, Simba yawaandalia dozi
Mighty Wonderers kutua nchini leo, Simba yawaandalia dozi
1d ago
READ MORE β†’
Kibabage ameanza mazoezi mepesi
Kibabage ameanza mazoezi mepesi
1d ago
READ MORE β†’
Chama apotezea kelele za mitandaoni, aweka msimamo
Chama apotezea kelele za mitandaoni, aweka msimamo
1d ago
READ MORE β†’
Oura anaamini huu utakuwa msimu bora kwa Simba
Oura anaamini huu utakuwa msimu bora kwa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Septemba 10 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Septemba 10 2026
1d ago
READ MORE β†’