Baada ya kuwasili nchini Malawi jana, jioni kikosi cha Simba kilifanya mazoezi yake ya kwanza nchini humo kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya wenyeji wao Mighty Wonderers.
Leo Simba itakamilisha maandalizi yake ya mwisho kuelekea mchezo huo utakaopigwa kesho Jumapili, Septemba 06 saa 9 Alasiri.








