Mpya

Chama ajutia kuondoka Simba na kujiunga Yanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Sep 2026
Chama ajutia kuondoka Simba na kujiunga Yanga

Kiungo fundi wa Simba Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka' amefichua kilichojiri nyuma ya pazia alipoondoka Simba na kujiunga na Yanga msimu wa 2024/25.

Chama amesema lilikuwa tukio ililompa wakati mgumu na alifanya jitihada za kutaka kurejesha kila kitu alichopewa na Yanga lakini haikuwezekana kwa wakati huo.

Chama amefichua hayo kwenye mahojiano maalum na Fatema Dewji.

"Ukweli ni kwamba nilijuta sana kuondoka Simba, siku niliosaini mkataba Yanga haikuwa siku nzuri sana kwangu"

"Nilimpigiaa Rais wa Yanga na kumwambia narudisha kila kitu ili nirudi Simba lakini akakataa akasema haiwezekani kwa sababu kila shabiki na kila mtu anakusubiri Yanga"

"Namshukuru Mungu sikuchukua muda mrefu pale kwa sababu sijawahi kufikiria kwenda kucheza Yanga ilitokea tu."

"Nilikuwa kwenye wakati mgumu lakini ninachoweza kusema ni kwamba nimerudi Simba na siku niliyosaini Simba nilifurahi sana na hata familia yangu ilifurahi," alisema Chama

Hata hivyo Chama alirejea Simba kwenye usajili wa dirisha dogo msimu uliopita akitokea Singida BS ambayo aliitumikia kwa miezi sita baada ya kuondoka Yanga alikocheza kwa msimu mmoja.

Chama ameanza vyema msimu huu akiwa tayari amepachika mabao matatu kwenye ligi kuu ya NBC.

More Stories

Simba yakamilisha maandalizi dimba la Uhuru
Simba yakamilisha maandalizi dimba la Uhuru
4h ago
READ MORE β†’
Libasse ameweka kabatini tuzo ya kwanza ya ligi kuu msimu huu
Libasse ameweka kabatini tuzo ya kwanza ya ligi kuu msimu huu
7h ago
READ MORE β†’
Mighty Wonderes wawasili Dar usiku
Mighty Wonderes wawasili Dar usiku
11h ago
READ MORE β†’
Makgalwa ajipa muda zaidi Simba
Makgalwa ajipa muda zaidi Simba
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
14h ago
READ MORE β†’
Mighty Wonderers kutua nchini leo, Simba yawaandalia dozi
Mighty Wonderers kutua nchini leo, Simba yawaandalia dozi
1d ago
READ MORE β†’
Kibabage ameanza mazoezi mepesi
Kibabage ameanza mazoezi mepesi
1d ago
READ MORE β†’
Chama apotezea kelele za mitandaoni, aweka msimamo
Chama apotezea kelele za mitandaoni, aweka msimamo
1d ago
READ MORE β†’
Oura anaamini huu utakuwa msimu bora kwa Simba
Oura anaamini huu utakuwa msimu bora kwa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Septemba 10 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Septemba 10 2026
1d ago
READ MORE β†’