Stars kuivaa Uganda ikiwa na matumaini kibao

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Sep 2018
Stars kuivaa Uganda ikiwa na matumaini kibao
Kikosi cha timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars), kimewasili salama jijini Kampala jana tayari kwa mchezo dhidi ya Uganda Cranes hapo kesho.

Nahodha wa timu hiyo, mshambuliaji, Mbwana Samatta, amesema kuwa hawana hofu yoyote kuelekea mchezo huo.

Mechi hiyo kati ya Uganda Cranes dhidi ya Taifa Stars ambayo ni ya kuwania tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon), itachezwa kesho kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Nelson Mandela (Namboole).

Samatta, amesema kuwa wachezaji wote wa timu hiyo wako tayari kwa mchezo huo na wanachoomba ni kutumia vyema nafasi ambazo watazitengeneza.

Samatta amesema wamejiandaa kukutana na ushindani na kuongeza kuwa hilo linatokana na wachezaji wa timu hizi mbili kufahamiana vizuri na baadhi ya Waganda kucheza katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

"Hii ni mechi muhimu sana kwetu, tunahitaji ushindi ili tuwe katika nafasi nzuri kwenye kundi letu, tunajua tunacheza ugenini lakini hiyo haitusumbui, tumejipanga kujituma kwa nguvu zetu zote," alisema Samatta ambaye anacheza soka la kulipwa katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.

Alisema kuwa wanaamini watajituma ili kupata ushindi na "kuamsha" matumaini ya kusonga mbele katika safari hiyo ya kusaka tiketi ya kucheza fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Naye mshambuliaji wa Al Hilal ya Sudan, Thomas Ulimwengu, amesema kuwa amerejea katika kiwango chake na anaamini atapambana kuhakikisha Stars inapata matokeo mazuri katika mechi hiyo.

"Namshukuru Mungu nimepona majeraha niliyokuwanayo na sasa niko fiti kuisaidia nchi yangu, najua changamoto iliyoko mbele yetu, lakini tunaahidi tutafanya kila linalowezekana ili kuwapa furaha Watanzania," alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa TP Mazembe.

Mechi ya kesho itakuwa ya kwanza kwa Kocha Mkuu mpya wa Stars, Mnigeria, Emmanuel Amunike, ambaye alitua nchini mapema Agosti kurithi mikoba iliyoachwa na Mzalendo, Salum Mayanga

Kama Stars itashinda mchezo huo au hata kupata sare itajiweka katika nafasi nzuri kundi L ambalo pia linazijumuisha Uganda, Lesotho na Cape Verde.

Uganda inaongoza kundi ikiwa na alama tatu ikifuatiwa na Stars na Lesotho ambazo zote zina alama moja.

Cape Verde ambayo itachuana na Lesotho kesho inashika mkia ikiwa haina alama.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
15h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
15h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
18h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’