Timu ya AFC Leopards kutoka nchini Kenya inatarajiwa kuwasili leo jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba Sc kesho Jumamosi.
Mkuu wa Habari wa Simba Haji Manara amesema wageni wao hao watawasili leo asubuhi na baadae watafanya wote Mkutano na waandishi wa habari.
"Kesho (leo) saa tano kamili asubuhi klabu za Simba na AFC Leopards ya Kenya, kwa pamoja zitaongea na waandishi wa habari za michezo kwenye ofisi za Shirikisho la Soka nchini TFF zilizopo Karume maeneo ya Ilala"
"Mazungumzo hayo yanalenga kuelezea Mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaopigwa siku ya Jumamosi ya tarehe nane pale kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
"Mabosi wa mabenchi ya ufundi ya timu zote na manahodha wao pia watakuwepo kwenye mkutano huo," imesema taarifa ya Manara

ADVERTISE HERE