Kocha Mkuu wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba Patrick Aussems ameeleza kushangazwa na taarifa zinazoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kuwa hana maelewano mazuri na Kocha Msaidizi wa timu hiyo Masudi Djuma.
Aussems amesema amekuwa akielezwa juu ya taarifa hizo zinazoripotiwa na magazeti, mitandao ya kijamii lakini amesisitiza kuwa hana tofauti yoyote na Djuma.
Tangu wiki iliyopita baadhi ya magazeti yamekuwa yakiripoti kuwa Aussems ambaye ameiongoza Simba katika michezo miwili ya ligi na kufanikiwa kushinda yote amekuwa hana maelewano mazuri na Djuma.
Aussems anadaiwa kupeleka malalamiko kwa uongozi wa Simba juu ya kutofurahishwa na tabia ya Djuma ya kumsaliti kwa kuwaambia wachezaji wa timu hiyo wacheze chini ya kiwango ili afukuzwe na Djuma achukue nafasi ya kuwa Kocha Mkuu.
Mkuu wa Idara ya Habari ya Simba Haji Manara alikanusha kuwepo kwa taarifa hizo ingawa bado zimeendelea kuripotiwa na magazeti karibu yote ya michezo.

ADVERTISE HERE