Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mbwana Samatta amewasili usiku wa kuamkia leo kujiunga na kikosi cha kocha Emanuel Amunike kinachojiandaa na mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019.
Samatta ameambatana na Thomas Ulimwengu anayekipiga na klabu ya El Hilal ya nchini Sudan.

Stars itasafiri nchini Uganda Septemba 08 kuwavaa ndugu zao kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, Uganda Cranes.
Wakati huo huo Winga Saimon Msuva anatarajiwa kutua leo kuungana na mastaa wengine wanaosakata kabumbu nje ya nchi tayari kwa mchezo huo.
Kikosi cha Stars kimeendelea kujifua ambapo jana jioni walifanya mazoezi kwenye uwanja wa Boko Vererans jijini Dar es salaam

ADVERTISE HERE