Simba imeendelea kujifua uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu unaofuata ambao utapigwa Septemba 15 dhidi ya Ndanda FC mkoani Mtwara.
Kocha wa viungo Adel Zrane amekuwa akiwapa wachezaji mazoezi maalum kuhakikisha wanakuwa na pumzi na stamina ya kutosha.
Simba imeanza ligi kwa kuibuka na ushindi kwenye michezo yake miwili ya kwanza dhidi ya Prisons na Mbeya City.
Hata hivyo kwenye michezo hiyo kikosi cha Simba kilionekana kupunguza kasi hasa kipindi cha pili michezo hiyo ilipokuwa ikielekea ukingoni.
Baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City, Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems aliahidi kuifanyia kazi changamoto hiyo kuhakikisha timu yake inacheza kwa nguvu kwa dakika zote tisini na kupata ushindi mnono zaidi.

ADVERTISE HERE