Aussems amepania, mazoezi ya Simba yamenoga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Sep 2018
Aussems amepania, mazoezi ya Simba yamenoga
Licha ya kushinda michezo miwili ya kwanza ya ligi, Simba umeuanza msimu huu taratibu tofauti na msimu uliopita hivyo kuibua hofu miongoni mwa mashabiki.

Lakini kocha Mkuu wa Simba Aptrick Aussems amesema makali ya mabingwa hao watetezi yataendelea kuongezeka.

Simba imeendelea kujifua kwa nguvu kwenye uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ndanda FC utakaopigwa mkoani Mtwara Septemba 15.

Simba inajifua ikiwa na kikosi kinachowakosa wachezaji watano Aishi Manula, Haruna Niyonzima, Cletus Chama, Meddie Kagere na Emanuel Okwi ambao wameitwa kwenye timu za Taifa.

Aidha kuondolewa kwa wachezaji sita wa Simba kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, imekuwa faida kwa Simba kwani sasa wana uhakika watakwenda mkoani Mtwara kuikabili Ndanda FC wakiwa na kikosi imara kisichokuwa na uchovu.

Kabla ya uamuzi huo Simba ilikuwa na wachezaji 12 walioitwa kwenye timu za Taifa.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
1h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
21h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
2d ago
READ MORE β†’