Fomu za uchaguzi Simba kuanza kutolewa leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Sep 2018
Fomu za uchaguzi Simba kuanza kutolewa leo
Baada ya Kamati ya Uchaguzi kutangaza rasmi tarehe ya uchaguzi Mkuu wa klabu ya Simba kuwa ni Novemba 03 2018, fomu kwa ajili ya wagombea zitaanza kutolewa kesho.

Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Uchaguzi mapema leo kupitia kwa Mwenyekiti wake, Boniphace Lihamwike imesema kwamba fomu za kugombea zitaanza kutolewa kesho Jumatatu kuanzia Saa 4:00 makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi.

Uchaguzi huo utafanyika kwa mujibu wa Katiba ya klabu ya Simba iliyofanyiwa marekebisho mwaka huu 2018.

Miongoni mwa nafasi zinazogambiwa ni ya Rais wa klabu ya Simba ambapo Katiba imeelekeza kuwa mgombea wa nafasi hiyo ni lazima awe na elimu ya kiwango cha Shahada ambaye ataongoza Bodi ya Wakurugenzi itakayokuwa na Wajumbe wanane chini yake.

Na Mwenyekiti huyo atakuwa na mamlaka ya kuteua Wajumbe wengine wanne, kati yao mmoja lazima awe mwanamke ili kukamilisha Bodi ya Ukurugenzi ya watu wanane.

Mkuu wa Habari wa klabu ya Simba Haji Manara amewataka wanachama wa klabu hiyo ambao wana sifa tajwa wajitokeze kuchukua fomu kuanzia kesho.

"Kesho tunaanza kutoa fomu za wanaoomba uongozi Simba. Nawasihi Wanachama jitokezeni kwa wingi kugombea.
Nafasi zitakazogombewa ni Mwenyekiti na Wajumbe watano wa Bodi ya Wakurugenzi," amesema Manara.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
13h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’