Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi tayari ameripoti kambi ya timu ya Taifa ya Uganda inayojiandaa na mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu AFCON 2019 dhidi ya Tanzania utakaopigwa nchini Uganda Jumamosi ijayo.
Okwi ameanza mazoezi baada ya kuwa nje kwa karibu wiki moja kutokana na maumivu ya mgongo aliyopata kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba dhidi ya Mtibwa Sugar mkoani Mwanza.
Mshambuliaji huyo mwenye rekodi hatari ya kupachika mabao anatarajiwa kuiongoza Uganda dhidi ya Stars katika mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka ukanda wa Afrika Mashariki.

ADVERTISE HERE