Simba leo inashuka uwanja wa KMC Complex kufunga hesabu za msimu huu kwa mchezo dhidi ya KMC.
Mpango wa Simba ni kuhitimisha msimu kwa ushindi mnono huku wakifahamu kimahesabu bado wana nafasi ya kutwaa ubingwa.
Leo mpango wa Simba uko wazi, kufunga msimu kibabe kwani lolote linaweza kutokea.
Ni siku nyingine kwa Mnyama kuendeleza rekodi tamu ya kocha Steve Barker ambaye kikosi chake hakijapoteza mchezo wowote tangu alipotua.
Tukutane KMC COMPLEX saa 10 jioni.