Kikosi cha Simba kimeondoka leo asubuhi mjini Mbeya kwenda Katavi mkoani Rukwa kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji wao.
Mratibu wa Simba SC, Abbas Suleiman amesema kwamba wanakwenda Katavi kwa mchezo mmoja wa kirafiki utakaochezwa kesho na Jumatano watarejea Mbeya.
Simba SC ambayo jana ilirudi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, itakuwa na mchezo mwingine wa Ligi Kuu mkoani hapa dhidi ya Tanzania Prisons Novemba 18.

ADVERTISE HERE