Mashabiki wa Simba wametolewa wasiwasi juu ya hatima ya mshambuliaji wao, Adam Salamba, wanayetamani kumwona akifanya mambo kikosini mwao kwa kuambiwa kuwa mkali huyo aliyetokea Lipuli ya Iringa ana kazi maalumu.
Salamba ni miongoni mwa wachezaji wapya wa Simba waliotua Msimbazi mwishoni mwa msimu uliopita, akiwa ameitumikia vema timu yake hiyo mpya kwa kufunga mabao matano katika mechi za michuano ya Kombe la Kagame na za kirafiki nchini Uturuki.
Kutokana na makali yake hayo, Salamba alikuwa akitajwa kama mchezaji mwenye uwezo wa kuibeba Simba katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, sambamba na nyota wengine wapya kama Meddie Kagere, Hassan Dilunga, Cletus Chama, Pascal Wawa na wengineo.
Lakini straika huyo hadi sasa hajacheza mechi yoyote kati ya mbili za Ligi Kuu Bara ambazo timu yake imecheza na kushinda zote dhidi ya Tanzania Prisons (1-0) na Mbeya City (2-0).
Badala yake, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amekuwa akiwatumia John Bocco na Kagere kama washambuliaji wa kati, huku nyuma yao kukiwa na viungo, Dilunga, Shiza Kichuya, James Kotei, Muzamir Yassin na Said Ndemla.
Hata hivyoAussems amesema kulingana na mfumo wake, anakuwa na utaratibu wa kuwapanga washambuliaji wake kutokana na mechi husika.
Aussems amesema Salamba ni mchezaji mwenye kipaji na makini anapokuwa uwanjani, hivyo kwa kuwa tayari alishapangwa katika mechi kadhaa zilizopita, kwa sasa amempa kazi maalumu ya kukusanya nguvu tayari kuipigania timu yake hiyo katika mechi zinazohitaji mshambuliaji wa aina yake.
โSalamba kiwango chake ni bora, amecheza mechi nyingi na amefanikiwa kufunga mabao, sioni sababu ya kumpanga kikosi cha kwanza kila mechi, naweza kumchosha mapema, mchezaji mzuri hupewa nafasi ya kupumzika ili mwili ukae fiti.
โKwa muda mfupi ambao nimekuwa naye (Salamba), nimeweza kumtambua kuwa ni mchezaji ambaye ana kiu ya kufanya vizuri na huwa anajituma sana akiwa uwanjani kuhakikisha anaisaidia timu yake kwa kufunga mabao. Nina imani nitakapompanga tena, atafanya vizuri zaidi,โ alisisitiza Mbelgiji huyo.
Aussems, alisema kutokana na uzoefu wake katika soka, anapoanza kukinoa kikosi kipya, huwa anasoma tabia na uwezo wa kila mchezaji hali ambayo inamsaidia jinsi ya kuwapanga, jambo ambalo tayari ameshalifanya kwa mchezaji huyo.
Aussems alisema kwa kuwa umri wa mshambuliaji huyo bado mdogo, anayo nafasi kubwa ya kuendelea kufanya vizuri na kuibeba mno Simba.
Mwenyewe Salamba amesema hana hofu na kutocheza sasa akiamini hali hiyo inamsaidia kujifunza kile ambacho wenzake wanakifanya uwanjani na kurekebisha makosa yake.
โKikosi chetu kina wachezaji wazuri tena wakongwe ambao nimewakuta, hivyo sina hofu na hilo, kwa kuwa najifunza kutoka kwao, ila natambua uwezo wangu hata nikipangwa kila siku ninaweza kufanya vizuri,โ alisema Salamba
Bingwa

ADVERTISE HERE