Ishu ya wachezaji Simba kuondolewa Stars, viongozi kupelekwa Kamati ya Maadili

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Aug 2018
Ishu ya wachezaji Simba kuondolewa Stars, viongozi kupelekwa Kamati ya Maadili
Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema viongozi wa Simba, Meneja Richard Robert na Kaimu Katibu Mkuu Hamisi Kisiwa wataitwa kwenye kamati ya Maadili kwa kuchelewa kuwapa taarifa wachezaji kuingia kambini licha ya Klabu hiyo kupewa taarifa na TFF mapema.

Uamuzi wa Kocha Mkuu wa Stars Emanuel Amunike kuwaondoa kikosini wachezaji wa Simba isipokuwa Aishi Manula umewashangaza wadau wengi wa soka nchini hasa baada ya wachezaji kubainisha kuwa hawakuwa wamepewa taarifa ya kuhitajika kambini jana.

"Kwa tafsiri ya kawaida kwenye maelezo ya Katibu Mkuu maana yake kosa sio la wachezaji bali ni la Uongozi wa SImba SC," amesema mmoja wa wachambuzi mahiri wa soka nchini Oscar Oscar.

"Maana yake wachezaji walioondolewa wamepewa adhabu ambayo hawakustahili.

"Naendelea kusisistiza kulikuwa na haja ya kuwasikiliza kwanza wachezaji kabla hata ya kuwahukumu moja kwa moja.

"Sio rahisi kwa wachezaji SITA wa Klabu moja, wote kutofika Kambini. Hawa wachezaji walipaswa kusikilizwa Kwanza, kuwaengua hakuwezi kumaliza tatizo".
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’