Simba yatoa wachezaji 12 timu za Taifa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Aug 2018
Simba yatoa wachezaji 12 timu za Taifa
Jumla ya wachezaji 12 kutoka klabu ya Simba wameitwa na timu za mataifa yao kwa ajili ya michezo ya kufuzu kwa michuano ya AFCON 2019.

Wachezaji saba wameitwa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambao ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Hassani Dilunga, Shiza Kichuya na John Bocco.

Haruna Niyonzima na Meddie Kagere wameitwa timu ya Taifa ya Rwanda, Emanuel Okwi na Juuko Murshidi wameitwa timu ya Taifa ya Uganda wakati Cleotus Chama ameitwa timu ya Taifa ya Zambia.

Akizungumzia kuitwa kwa wachezaji hao, Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema tukio hilo limeipa heshima kubwa Simba.

"Uongozi wa Simba unaendelea kuwashukuru watanzania kwa kuendelea kuiunga mkono timu yetu na niwafahamishe tunasonga mbele, haturudi nyuma," amesema Manara.

"Pia tunawashukuru Makocha wa timu za Taifa za Tanzania, Rwanda,Uganda na Zambia kwa kuteua wachezaji 12 kutoka Simba kujiunga na timu zao za Taifa.

"Ni heshima kwa klabu yetu na tutatoa ushirikiano mkubwa kwao"
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’