Waamuzi 'walioboronga' wasimamishwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Aug 2018
Waamuzi 'walioboronga' wasimamishwa
Kamati ya Waamuzi ya shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa mwenyekiti wake Mzee Salum Chama imewasimamisha baadhi ya waamuzi ambao wameboronga kwenye michezo ya raundi ya kwanza na ya pili ya ligi kuu Tanzania Bara (TPL).

Waamuzi waliosimamishwa kupisha uchunguzi mwamuzi msaidizi namba 2 (Line 2) Godfrey Msakila kutoka Geita mchezo kati ya Yanga SC dhidi Mtibwa Sugar, Msakila anadaiwa kukataa goli la Makambo kwa kudai mfungaji alikuwa kwenye eneo la kuotea.

Mwamuzi mwingine ni Sylvester Mwanga kutoka Kilimanjaro (Line 1) mchezo wa Yanga dhidi ya Mtibwa naye amesimamishwa kwa kulalamikiwa kuzuia shambulizi la Mtibwa akidai Ismail Aidan alikuwa ameotea huku picha za video za marudio ya tukio hilo zikionyesha hakuotea.

Pia refa wa kati Nassoro Mwinchui na msaidizi wake Abdallah Rashid wa Pwani wamesimamishwa kwa kosa la kukataa goli la Biashara United katika mechi ya Coastal Union dhidi ya Biashara wakidai mfungaji alikuwa ameotea.

Wengine ni Mwamuzi msaidizi Nicholas Makaranga wa Morogoro amesimamishwa kwa kukataa goli la Ruvu Shooting dhidi ya KMC akidai mfungaji Fully Zullu Maganga alikuwa kwenye nafasi ya kuotea.

Pia Rungu hilo la kusimamiahwa limemkuta msaidizi Ahmada Jamada kutoka Kagera ambaye alikataa goli la kusawazisha la Mwadui FC dhidi ya Singida United juzi Jumapili kwa madai ya kuwa mfungaji alikuwa ameotea

Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mzee Salum Chama alisema waamuzi hao walichezesha chini ya kiwango na kupata Alama chache zilizopelekewa kusimamishwa kupisha uchunguzi kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi.

Kamati ya uendeshaji wa ligi ya Tanzania Bara (Kamati ya saa 72) itakaa na kufanya uchunguzi na itatangaza hatua zaidi watakazochuliwa iwapo uchunguzi utabaini marefa walifanya makosa katika mechi hizo.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
30m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’