Manara akanusha tetesi za Djuma kuondoka Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Aug 2018
Manara akanusha tetesi za Djuma kuondoka Simba
TAARIFA YA MANARA KUHUSU TETESI ZA DJUMA

Leo nimepigiwa cm nyingi toka kwa waandishi wa habari na washabiki wa Simba kutaka kujua ukweli wa taarifa zilizoandikwa kwenye gazeti moja likidai kocha msaidizi wa Simba anaondoka baada ya kutofautiana na kocha Mkuu Patrick Aussems.

Kocha huyo Masoud Djuma inaarifiwa pia eti amekosana na baadhi ya wachezaji wetu.

Simu hizo zimeambatana na msg nyingi za WhatsApp na sms pamoja na kwenye page yangu ya Instagram.

Hakuna niliyemjibu zaidi ya kuchukizwa na tabia ya baadhi ya watu kukubali kila porojo inayoandikwa ama kwenye baadhi ya magazeti au mitandaoni.

Ieleweke hakuna atakaekaa Simba milele si Masoud au Aussems na hata mm ninaendika hii makala fupi,lakini wote tutaondoka pale muda wetu utakapofika na kwa utaratibu maalum

Sasa huku kwenye michezo..bado kuna dhana potofu Mwandishi anaweza kuandika lolote na chochote anachojisikia bila kuulizwa wala kuchukuliwa hatua na ndio maana leo story za kupikwa zimekuwa nyingi kupita maelezo

Na umezuka mtindo inapikwa story kisha ndio unaulizwa eti ili ubalance story!!

Haji huwa hahangaiki na kubalance porojo na hekaya..Haji anashughulikia mambo ya msingi ya maendeleo ya Taasisi.

Na ukitaka kuamini hzo cooked stories zote hazina sources zinawekwa kusudi kwa dhamira zao..na hazibalansiwi kwanza..zinaandikwa kisha ndio tunaulizwa!!

Narudia tena na tena kabla ya kupika hzo porojo ni vema mkabance kwanza kama taaluma inavyotaka kuliko kuandika kisha mwandishi wa gazeti hilo hilo anataka kubalance!!

Na kwa mashabiki wetu si kila kinachotoka migodini ni madini mengine ni michanga tu kama iliyopo ardhini,walau ingekuwa Makanikia!!

Nimalizie kwa kuwaambia Simba ni shwari na kilichoandikwa ni hekaya na hadithi sawa na zile za Abunuwasi..tusitolewe mchezoni kirahisi rahisi..tuendelee kuwa wamoja na tusiyumbishwe kwa maneno ya mahotelini

Mkata Vimeo
De Le Boss
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
30m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’