Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema anaamini mshambuliaji wake John Bocco 'Adebayor' atarejea kwenye kiwango chake cha kutupia nyavuni.
Bocco ameanza msimu vibaya kutokana na kusumbuliwa na majeruhi yaliyomfanya akose michezo ya maandalizi ya msimu mpya.
Alicheza mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Prisons lakini alionyesha dhahiri kuwa bado hajarejea kikamilifu kama ilivyokuwa msimu uliopita.
Akizungumzia hali hiyo, Aussems amesema ni kawaida kwa mchezaji anayetoka majeruhi kurejesha taratibu uwezo wake.
"Bocco ametoka kwenye majeruhi, anahitaji muda zaidi kuweza kurejesha makali yake."
Kuumia kwa Bocco kumemfanya Aussems awatumie Okwi na Kagere kama washambuliaji wa kwanza.
Adam Salamba na Mohammed Rashidi ni washambuliaji wengine ambao wamekuwa wakitumiwa kwa dharura na kocha Aussems.

ADVERTISE HERE