Bao la Shiza Kichuya alilofunga kwenye dakika ya saba kipindi cha kwanza limeiwezesha Simba kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kuichapa Mbeya City bao 1-0.
Pasi murua ya kiungo Jonas Mkude ilitendewa haki na Kichuya aliyewatoroka walinzi wa Mbeya City na kuukwamisha mpira wavuni kwa urahisi.
Simba ilicheza kandanda safi na hakika ushindi ni matokeo stahili.
Baada ya ushindi huo Simba imefikisha alama 19 na kuiondoa Azam FC kileleni.
Licha ya timu zote kuwa na alama sawa, Simba imefunga mabao mengi zaidi kuliko Azam FC.
Mchezo mwingine uliopigwa leo kati ya Lipuli na Mwadui FC umemalizika kwa sare ya bao 1-1.

ADVERTISE HERE