Niyonzima kurejea kikosini Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Aug 2018
Niyonzima kurejea kikosini Simba
Kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha mabingwa wa Tanzania Bara Simba baada ya kumalizana na uongozi wa timu hiyo, imefahamika.

Kumekuwa na sintofahamu inayoendelea 'chinichini' kati ya Niyonzima na uongozi wa Simba ambayo imepelekea kiungo huyo mnyumbufu 'kugoma' kurejea kikosini.

Niyonzima aliyesajiliwa na Simba akitokea klabu ya Yanga msimu uliopita anadai kutotimiziwa baadhi ya makubaliano ya mkataba na uongozi wa Simba.

Hata hivyo sintofahamu hiyo imemalizika na Niyonzima wakati wowote atarejea kuendelea kuitumikia Simba katika msimu wake wa pili.

Kurejea kwa Niyonzima kikosini kutaimarisha zaidi safu ya kiungo cha ushambuliaji cha Simba ambacho tayari kina wapiga mpira wakali kama Cleotus Chama na Hassani Dilunga.

Hata hivyo Niyonzima itabidi afanye kazi ya ziada kuweza kurejea kwenye kikosi cha kwanza kutokana na uhodari wa viungo hao.

Niyonzima na Meddie Kagere wameitwa kwenye kikosi cha Rwanda kinachojiandaa na michuano ya kufuzu AFCON 2019.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’