Wawa afurahia 'combination' yake na Nyoni

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Aug 2018
Wawa afurahia 'combination' yake na Nyoni
Beki kisiki wa Simba Paschal Wawa, amefurahia kombinesheni yake na Erasto Nyoni na kutamka kuwa itawasumbua washambuliaji wa timu pinzania kupenya ngome yao.

Wawa alianza kwa kiwango cha kusuasua kwenye mechi za kirafiki lakini ameonekana kuanza kuimarika kadri anavyopewa mechi nyingi za kucheza hasa anapopangwa na Nyoni ambaye waliwahi kucheza wote Azam.

β€œMimi na Nyoni tunafahamiana muda mrefu kwahiyo tunapocheza tunakuwa na lengo moja tu la kuhakikisha tunaisaidia timu yetu iweze kufanya vizuri, nashukuru Mungu tumetoka na ushindi,” alisema.

Akizungumzia ugumu wa washambuliaji wa Ligi Kuu, alisema ni hali ya kawaida kwa mshambuliaji yoyote kutaka kufunga, lakini umakini wa mabeki ndio unaweza ukafupisha safari yao.

β€œNajua washambuliaji wanataka kupata magoli kila mara ndio maana na mimi napambana vilivyo kuhakikisha kwamba nakuwa fiti kupambana nao, kazi yao ni kufunga na sisi kuzuia,” Wawa aliliambia gazeti la Mwanaspoti

Beki huyo raia wa Ivory Coast amejihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Patrick Aussems akiwa mpaka sasa ameanza kwenye michezo yote muhimu ya Simba.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
30m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’