Tunaendelea kuimarika - Bocco

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Aug 2018
Tunaendelea kuimarika - Bocco
Nahodha wa Simba, John Bocco amesema mwanzo wa ligi unakuwa wa ushindani wa hali ya juu na kadri siku zitakavyokuwa zinaendelea ndivyo watakavyopata ya picha ya nini wanatakiwa kufanya ili waweze kutetea ubingwa.

Bocco alisema kitendo cha kuanza na ushindi dhidi ya Prisons kimewaongezea kujiamini na kuendelea kutamani kushinda kila mechi.

"Mechi za ufunguzi timu zinakuwa zimepania, kwani zinakuwa zimetoka kwenye maandalizi, ndio maana hata mchezo wetu na Prisons, ulikuwa mgumu na waushindani mkubwa.

"Pia tunaamini tutashinda dhidi ya Mbeya City ambayo tunatarajia kucheza nayo, Jumatatu wiki ijayo, tunajipanga kwa ushindani wa hali ya juu kwani si timu ya kubeza,"alisema Bocco.

Amewaomba mashabiki wa timu hiyo kuendelea kujitolea kufika uwanjani kila wanapokuwa wanacheza akisema watafanya vitu ambavyo vitawafanya wawe wanaondoka na tabasamu.

"Kiu ya shabiki ni ushindi, nguvu yao ya kutuunga mkono itatusaidia kutupa moyo kujua tuna deni la kuwalipa pindi wanapokuwa wamefika uwanjani kuishangilia timu yao, wajitoe kwa bidii na sisi tutafanya kwa bidii katika sekta inayotuhusu," alisema Bocco.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’