Aussems ataja sababu ya kutomtumia Okwi mchezo dhidi ya Prisons

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Aug 2018
Aussems ataja sababu ya kutomtumia Okwi mchezo dhidi ya Prisons
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi ameshindwa kucheza katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prison jana kwenye Uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo Simba ilishinda bao 1-0 lililofungwa dakika ya pili na mshambuliaji Meddie Kagere aliyepokea pasi safi ya kisigono kutoka kwa nahodha John Bocco.

Okwi mfungaji bora wa msimu uliopita alikosekana mechi hiyo kutokana na kuwa na maumivu ya mgongo ambayo aliumia katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kocha wa Simba, Mbeligiji Patrick Aussems alisema ameshindwa kumpa nyota huyo nafasi ya kucheza kwa kuwa ana maumivu ya mgongo na bado hajapona vizuri na kama angelazimisha kumtumia angeweza kumkosa muda mrefu.

Aussems alisema Okwi aliumia mgongo katika mechi ya Mtibwa ambayo alishindwa kuendelea na alitoka nje maumivu ambayo anatakiwa kupata matibabu huku akipata muda mwingi wa kupumzika ili kupana haraka.

Anasema Okwi anaendelea vizuri na matibabu na alikuwa na uwezo wa kumtumia katika mechi hiyo, lakini kwa kuwa walikuwa mbele kwa bao moja aliona vyema kumpumzisha ingawa alikuwa katika benchi la wachezaji wa akiba.

"Tuna mechi nyingi mbele yetu zinakuja ningeweza kumtumia akaja kutonesha maumivu au kuumia zaidi na tukamkosa kwa muda mrefu jambo ambalo lisengekuwa sahihi kwetu," alisema kocha huyo.

"Kikosi ni kipana kukosekana kwa Okwi nafasi yake amecheza mchezaji mwingine," alisema Aussems

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
29m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’