Licha ya Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 jana dhidi ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania Bara, kumekuwa na ukosoaji mkubwa miongoni mwa mashabiki wa Simba ambao hawakuridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na mabingwa hao hasa kwenye kipindi cha pili.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ameshangazwa na hali hiyo licha ya kuwa Simba ilihitaji alama tatu kwenye mchezo huo na ilifanikiwa kuzipata.
"Wakati mwingine najiuliza nn wanadaamu wanataka?hasa washabiki wa Mpira," ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.
"Nimetalii kdogo kwenye magroup machache ya Wanasimba kwenye WhatsApp nimeshangaa baadhi yetu kutokuridhika na ushindi wa leo wa goli moja dhidi ya Prisons!
"Wengine kwenye Instagram wanafika mbali zaidi eti mfumo wa kocha haufai!! Guys mpira ni sayansi kubwa kuliko kwenda mwezini au daktari kumfanyia upasuaji wa kichwa mtu.
"Ukubwa wa Sayansi hii ni kwamba hujui mpinzani wako kajipangaje. Hujui kama siku hyo wachezaji wako watacheza kwa kiwango gani lakini kubwa Sayansi hii haina jawabu la moja kwa moja kama hesabu.
"Hisabati 3Γ3 ni tisa tu..hata ukokotoe vipi! Huku kwetu kwenye ndiki 3Γ3 inaweza kuwa bilioni nane
"Mara nyingi huwa nakataa kuwepo kwenye groups za WhatsApp sababu asilimia kubwa mpira wameujulia mitandaoni.
"Hawana shibe ya mchezo huu adhimu kabisa!!
Kwao hudhani kila siku Simba itashinda na kwao ushindi ni lazma upate goli saba au tano..kwao ushindi ni mnono tu..hata kama unakutana na Wanaume wenzako!
"Wanabeza huku wakisahau Prisons iliingia top four Msimu uliopita,wanabeza huku wakijua Prisons haifungwi kitoto kama Mnyela United!
"Halafu wanakuja na hoja dhaifu inayopaliliwa na wanazi wa nazi chai eti team imetoka Uturuki why ishinde moja? Afana aleik!!
"Hapo ndio Haji naonekana mtata..aliowaambia tulienda Uturuki kujifunza mpira ni nani? Kule tulienda camp ya pre season.ni mazoezi ya mwanzo wa msimu
"Wengine walienda Zanzibar kama Prisons na wapo walioenda hadi Mkamba..kote huko ilikuwa inatafutwa chemistry ya team toka kwa makocha.
"Ni lazima mnapoamua kuushabikia mchezo huu mjifunze sayansi yake na msijifunze sayansi hii kiwepesi wepesi kama mnajifunza Sayansi kimu
"Leo tumecheza na team nzuri na walijiandaa kama tulivyojiandaa cc..na lazma muelewe mfumo wa kocha hauingii kwa kipindi kifupi..unachukua muda kdogo..
"Niwasihi sana Wanasimba Soka ni zaidi ya mchezo wa draft au Chess ya kina kasparov na karpov..inahitaji shabiki kabla ya kulaumu ajue vtu vingi kdogo kwenye medula yake..vinginevyo ni kufanya uchale tu
"Sina maana tunakataa ushauri ila uwe ushauri unaoendana na taaluma na kama huna jijengee busara ya kupiga kimya..Usifate mkumbo wa mitandaoni"

ADVERTISE HERE