FT : Simba 1-0 Prisons

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Aug 2018
FT : Simba 1-0 Prisons
Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wameanza vyema kutetea taji lao baada ya kuichapa Tanzania Prisons bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa, Jumatano usiku.

Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi na ilijipatia bao mapema tu kwenye dakika ya pili mfungaji akiwa Meddie Kagere aliyepiga shuti lililotinga wavuni akiwa nje kidogo ya 18.



John Bocco alimpa pasi ya kisigino Kagere ambaye hakufanya ajizi na kuukwamisha mpira huo wavuni.

Simba ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi hasa kwenye kipindi cha kwanza ikikosa nafasi kadhaa za wazi.

Kwenye kipindi cha pili Tanzania Prisons ilirejea mchezoni na ilijaribu kusaka bao la kusawazisha bila ya mafanikio.



Katika kipindi hicho Kagere alikosa nafasi nyingine ya wazi ambapo mpira wake wa kichwa ulitoka sentimeta chache kwenye lango la Prisons.

Mchezo huo ulimshuhudia kiungo wa Simba Hassani Dilunga akilazimika kucheza na bandeji kichwani kabla ya kutolewa wakati mchezo ukielekea mwishoni baada ya kuuumia kwenye kipindi cha kwanza.



Ushindi huo umeifanya Simba iungane na timu za Mbao FC, Kagera Sugar, Biashara United na Ndanda FC ambazo zimeshinda michezo yao ya ufunguzi wa ligi.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
8h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
14h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
17h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’