Nahodha wa Simba, John Bocco amesema mechi yao dhidi ya Prisons itakuwa ngumu na ushindani wa hali ya juu, lakini watahakikisha wanapata ushindi mnono.
Simba mabingwa watetezi wa ligi hiyo, jambo lililomfanya Bocco aseme ili waendelee kutunza heshima hiyo, inawalazimu kwa hali na mali kuanza kwa kishindo kitakachofanya njia yao ya kutetea taji hilo iwe wazi.
"Tunatambua tunacheza na timu ngumu na yenye ushindani wa hali ya juu, hivyo tumejipanga kukabiliana nao, kuhakikisha tunashinda mechi hiyo lengo ni kujiweka katika mazingira sahihi ya kutetea ubingwa.
"Tunafahamu wazi kwamba msimu huu utakuwa wa tofauti kwanza namna timu zilivyosajili na pia ongezeko la timu na mechi, hilo linatufanya tujiweke sawa zaidi ili kuweza kukabiliana na hayo yote,"anasema.
Mbali na hilo amezungumzia namna alivyojipanga kuvunja rekodi ya kufunga mabao zaidi ya 14 ambayo aliyoyamiliki msimu uliopita, akisisitiza kwamba anahitaji kazi yake iwe bora kila wakati.
"Mguu wangu ndio ofisi yangu, lazima niboreshe kazi zangu ziwe bora, nimejipanga kuhakikisha nafunga mabao zaidi ya 14 kwani huu ni msimu mwingine lazima niwe na jipya," alisema Bocco.
Wakati Bocco akiyazungumza hayo, kocha wa Prisons, Abdallah Mohamed amejibu mapigo kwamba hakuna anachokihofia Simba.
"Sijaona maajabu yoyote Simba kama wao wataingiza wachezaji 11 basi na Prisons tutaingiza 11 kama ni maandalizi nimefanya ya kutosha na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kufanya kazi,"alisema Mohamed.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE