Niyonzima, Kagere waitwa timu ya Taifa Rwanda

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Aug 2018
Niyonzima, Kagere waitwa timu ya Taifa Rwanda
Licha ya kutofanya mazoezi na timu yake ya Simba, kiungo wa kimataifa Haruna Niyonzima, ameitwa katika kikosi cha timu ya soka ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) ambacho kitakutana na Ivory Coast Septemba 7, mwaka huu jijini Kigali.

Niyonzima amekuwa nje katika kikosi cha Simba tangu Juni mwaka huu na hakuwa pamoja na wachezaji wenzake walipokwenda Uturuki kuweka kambi ya wiki mbili kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Nyota mwingine aliyeitwa katika kikosi cha Amavubi anayecheza Tanzania ni mshambuliaji mpya wa Simba, Meddie Kagere ambaye alitua kwa mabingwa hao akitokea Gor Mahia ya Kenya.

"Ninafuraha na ninajua nini natakiwa kufanya, siko katika timu, lakini kama mchezaji sikuwa nimekaa kizembe," alisema Niyonzima, kiungo huyo wa zamani wa APR ya Rwanda na Yanga ya jijini Dar es Salaam.

Niyonzima alisema anaamini matatizo yake yatakwisha hivi karibuni na kurejea katika kikosi hicho ambacho Jumamosi kilitwaa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 2-1.

Amavubi na Ivory Coasta wanakutana katika mechi ya kusaka tiketi ya kucheza fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazochezwa mwakani.

Tanzania (Taifa Stars) yenyewe itasafiri kwenda kuivaa Uganda Cranes Kampala Uganda Septemba 6, mwaka huu
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’