Jana jioni kikosi cha Simba kilifanya mazoezi ya mwisho kabla ya mechi yao dhidi ya Mbeya City itakayopigwa kwenye dimba la Sokoine mkoani Mbeya leo.
Mazoezi hayo yalifanyika kwenye Uwanja huo utakaotumika baadae.
Kwenye mazoezi hayo, Omog alionekana kusimamia mazoezi ya wachezaji wake hasa viungo na washambulizi kuhakikisha wanapiga mashuti kila wanapopata nafasi.
Kocha huyo Mcameroon, alikuwa akiwasisitiza kulenga lango na waliokosea walirejea tena kuhakikisha wanafanya vizuri.
Simba inahitaji kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo ili iweze kurejea kileleni.
Kwa sasa Azam FC inaongoza ligi ikiwa na alama 19. Simba itafikisha alama hizo kama itaifunga Mbeya City.

ADVERTISE HERE