Juzi Jumamosi Simba ilitetea taji lake la Ngao ya Jamii kwa kuikamua Mtibwa Sugar, lakini kumbe hizo ni salamu za kocha wa timu hiyo, Mbelgiji Patrick Aussems kwa wapinzani wao katika Ligi Kuu Bara itakayoanza keshokutwa Jumatano.
Kocha Aussems anasema kubeba taji hilo ni mwanzo mzuri na kwamba wataenda kuendeleza moto katika Ligi Kuu wakianza kwa kuikaribisha Prisons Mbeya kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Mwanza, Kocha Aussems alisema baada ya kupambana na kutwaa Ngao, kwa sasa anaelekeza nguvu zake katika ligi ili kutetea taji lao.
βHizi ni salamu kuelekea Ligi Kuu, tunayo sababu ya kutetea tena ubingwa, tumejipanga na wachezaji wote wana ari ya ushindani, hivyo mashabiki wa Simba watarajie makubwa zaidi,β alisema Aussems.
Aliwaomba mashabiki wa Msimbazi kuendelea kuiunga mkono timu hiyo na kuwa na umoja ili kuiwezesha kufanya vyema kwenye mashindano yake.
Alisema kuwa Simba ina mechi nyingi zikiwemo za kimataifa, hivyo mafanikio yake yatatokana na sapoti ya mashabiki na wapenzi wake ili kufika mbali.
βVijana wapo tayari kwa kazi,β alitamba.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE